Copa ni Barcelona na A.Bilbao fainali

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jezi za wakali wa timu ya Barcelona, Messi na Neymar

Timu za Barcelona na Atletico Bilbao zitaumana katika fainali za kombe la Copa del Rey tarehe 30 Mei, baada ya kufuzu michezo yao ya nusu fainali iliyochezwa Jumatano usiku kwa michezo miwili ya nusu fainali.

Barcelona ilimenyana na Villarreal katika mchezo wa marudiano baada ya ule wa awali uliopigwa katika dimba la Barcelona la Nou Camp.

Katika kipute hicho cha jana Barcelona waliwafunga wapinzani wao mabao 3-1 na kuingia fainali kwa jumla ya mabao 6-2 katika michezo yote miwili iliyochezwa na timu hizo.

Nayo Atlhletico Bilbao ikaisasambua Espanyol bao 2-0 na kuweza kuingia fainali kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo uliopita.

Kwa matokeo hayo sasa Barcelona watavaana na Athletico Bilbao katika mchezo wa fainali utakaopigwa tarehe 30 Mei.