Kiazi mbatata kinazuia Mimba?

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kiazi husika

Msichana mmoja nchini Colombia ametoa kubwa na kali ya mwaka baada ya kukizamisha kiazi mbatata sehemu zake za siri na kiazi hicho kuanza kuchipua humo ndani, na binti huyo alifanya uamuzi huo kwa minajili ya njia ya uzazi wa mpango .

Unajiuliza? Kiazi mbatata ndio!

Haki miliki ya picha bbc

Binti huyo inakadiriwa kuwa ana umri wa miaka 22, na anaeleza wazi kuwa mama yake mzazi ndiye aliyemuonesha njia hiyo ya asili kwa amaelezo kwamba kiazi mbatata kinapoingizwa sehemu za siri ni njia nzuri ya uzazi wa mpango.

Ndio ni mamake mzazi.

Tatizo la binti huyo lilijitokeza wakati binti huyoalipokwenda clinic huku akilalamikia maumivu yasiyokuwa ya kawaida,na nesi alipomfanyia uchunguzi aligundua mizizi inayochipua ikichungulia kutoka kwenye sehemu zake za siri.

Baada ya kuzuru kliniki,na kupita wiki mbili kiazi kilianza kuota na kuchipua mizizi na kukua. Lakini kiazi hicho kiliondolewa na binti huyo hakupata athari zozote katika njia yake ya uzazi.

Njia zisizo sahihi na hatari za uzazi wa mpango bado zinaendelea kutumika ulimwenguni kote hasa na mabinti wadogo wanaojihusisha na ngono za utotoni.