Ronaldo huijali mno Sanamu yake .

Image caption Sanamu yenye matunzo ya Christian Ronaldo

Cristiano Ronaldo mara zote amekuwa na maamuzi ya kipekee yasiyo pitia kwa mtu wa pili na likija suala la kujijali ama kujipenda humwambii kitu hutekeleza ,suala ambalo limemfanya aonekane mchezaji wa kipekee mkubwa na imemjengea heshma kubwa.

Lakini mkali huyu wa kabumbu anayesukuma gozi Real Madrid katika kujipenda amepiga hatua moja mbele yenye kuzua mjadala katika mitandao ya jamii na miongoni mwa watu wanaomfahamu ,na kama kinachosema na mtunza makumbusho wa timu Real Madrid ambaye kazi yake kubwa ni utunzaji wa sanamu za wachezaji na kuhakikisha hazipauki na kubaki kama wachezaji halisi walivyo .

Gonzalo Presa, ndiye mhifadhi mkuu wa makumbusho hayo ya timu wa Real na ambaye pia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Museo de Cera ,ametema kwamba Ronaldo hutuma kinyozi wake binafsi mara moja kwa mwezi kuhakiki sanamu inayofanana naye iwe na muonekano anaoutaka.

Na anasema kwamba Cristiano huwa anataka sanamu hiyo ichanwe nywele mara moja kwa mwezi,na nywele za sanamu hiyo zimeagizwa kutoka nchini India ni nywele halisi .

Ronaldo mwenyewe ana makumbusho yake binafsi nchini Ureno,na makumbusho hayo yameendelea kuonesha mambo yamhusuyo tangu mwezi December,mwaka 2013.