Watu 5 wauawa katika klabu ya burudani

Image caption watu watano wauawa baada ya klabu ya burudani nchini Mali kushambuliwa

Watu watano wameuawa kwenye shambulizi la kigaidi kwenye klabu ya burudani katika mji mkuu wa Mali Bamako.

Raia mmoja wa Ufaransa aliuawa kwa kupigwa risasi kwenye klabu hiyo iliyo kwenye mtaa ulio na shughuli nyingi.

Mwandishi wa BBC eneo hilo anasema kuwa raia wawili wa Mali polisi na mlinzi mmoja pamoja na raia mwingine wa Ubelgiji waliuawa barabarani na washambuliaji waliokuwa wakitoroka.

Walioshuhudia walisema kuwa watu wanne walionekana wakitoroka kutoka eneo la mlipuko ambapo mmoja wao alisikika akisema kwa sauti Mungu ni mkuu kwa lugha ya kiarabu.