Raia wa Israel wampinga Netanyahu

Haki miliki ya picha GETTY
Image caption Raia wa Israel wafanya maandamano ya kupinga uongozi wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu

Watu zaidi ya 25 elfu wameshiriki kwenye mhadhara mjini Tel Aviv, kumpinga waziri mkuu, Benjamin Netanyahu ambapo walitaka mabadiliko katika mwelekeo wa siasa na uongozi wa Israel.

Meir Dagan, mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad, ameuambia mkusanyiko huo jana usiku, kuwa uongozi wa nchi hiyo unamtisha zaidi, kuliko anavyotishwa na maadui.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Benjamin Netanyahu

Mhadhara huo ulitayarishwa na shirika la raia, linalotaka makubaliano ya amani baina ya Israil na Wapalestina.

Waandishi wa habari wanasema hayo yalikuwa kati ya maandamano makubwa kabisa dhidi ya serikali, kufanywa kabla ya uchaguzi wa kati ya mwezi.