Mbwa anayegundua saratani kwa binaadamu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mbwa

Watafiti wa Marekani wanasema kuwa mbwa amefanikiwa kunusa ugonjwa wa saratani ya koromeo, yaani thyroid, ambayo wakaguzi walikuwa hawakuiona.

Mbwa huyo kutoka Ujerumani kwa jina Frankie alifundishwa kunusa mikojo ya watu walionao na wasiokuwa na ugonjwa huo.

Aliweza kugundua saratani ya mgonjwa mara 30 katika visa 34.

Wanasayansi wanaona hiyo inaweza kuwa njia mpya ya kukagua saratani hiyo ya koromeo, ama thyroid.

Wanasema huenda ikayasaidia maeneo tofauti duniani ambayo hayana vifaa vya kuugundua ugonjwa huo.