Ng'ombe amuua aliyekuwa akimzalisha

Image caption Ng'ombe aliyeua

Wakati mwingine wema unaweza kukuponza, ama wahenga wanasema tenda wema wende zako malipo kwa Mungu. Nayasema haya kwasababu mwanamke mmoja amekumbwa na ng’ombe na kusababisha kifo cha bibi huyo wakati akimsaidia azae .

Ajali hiyo imetokea katika shamba la mwanamke huyo Bixter, eneo la utafiti wa kilimo na mifugo huko Shetland, nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita.

Inaaminika mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 62 alikuwa akimsaidia ng’ombe wake azae na ndipo alipo kumbwa na mkasa huo

Polisi wa Scotland tayari wameanza uchunguzi wa ajali hiyo kupitia kitengo chao cha afya na usalama .