Pakistan yaibua vipaji

Image caption Saania na Muqqadas wakiwa na mama yao Shahnaz Tabaydar

Majirani zetu husimama katika milango,madirisha na hata paa za nyumba zao wakiizunguka nyumba ya Tabaydar katika eneo la watu wa maisha ya chini nje kidogo ya Lahore,nchini Pakistan,kauli ya mabinti waliotawala katika mitandao ya kijamii hivi sasa.

Na eneo lote linaonekana kama onesho la wazi hivi , kwani wanawake, wanaume na watoto huizunguka nyumba yetu wakitushangilia wengine wakisukumana kidogo ili kupata nafasi nzuri zaidi ya kutushuhudia wakati tukifanya mazoezi.

Mabinti hao wawili ambao wemezusha gumzo wa kwanza ana umri wa miaka kumi na mitano aitwaye Saania na wa pili ana umri wa miaka kumi na tatu anaitwa Muqqadas watoto wa Tabaydar na mtaani kwao wamepewa jina la utani wanajulikana kama 'Justin Bibis'.

Mabinti hao ambao ni ndugu wa baba mmoja wamegeuka kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii mara baada ya video inayowaonesha wakiimba wimbo wa msanii maarufu Justin Bieber's wakiimba wimbo uitwao Baby,cha kuvutia zaidi wanaimba na huku mama yao akiwapigia vyombo alichagua chungu video ambayo BBC meishuhudia.

Mama wa mabinti hao Shahnaz Tabaydar ,anakiri kwamba anampenda Justin Bieber sana na anajihisi kama ni mtoto wake wa kiume hivi.

Watu wa Pakistan wakaiweka hiyo video mtandaoni na kumchokoza Bieber wakimwambia amepata wapinzani wake hao mabinti wawili.

Mabinti hao Saania na Muqqadas wanasema walianza kuimba tangu walipokuwa na umri mdogo kabisa,lakini hili ni suala la kifamilia zaidi kwani walio wengi kwenye familia wanaimba pia.hatuimbi tungo za Bieber tu bali hata tungo za Pakistan na Bollywood anasema Saania.

Image caption Lugha ya Urdu ya Lahore.

Lakini tumezidia mapenzi yetu kwa Justin Bieber na hasa tungo zake kwasababu zimegusa mioyo yetu .Na mara tulipousikia wimbo wa Baby wa Justin, tukaanza kucheza na kuruka ruka na tukazama kifikra kabisa juu ya wimbo huu aliongeza Saania anayeonekana mzungumzaji mzuri tu.

Madada hao wamesha usikiliza wimbo huo mara sabini zaidi kuonesha mapenzi yao kwa tungo hiyo mwanana kabisa.wakiusikia wimbo huo tu ukichezwa popote, huwa wanazubaa na kushindwa kula ama hata kunywa chochote,huusikiliza tu,nikaanza kujifunza na kujifunza zaidi mpaka nilipoweza kuuimba wote kutoka moyoni .

Mabinti hao wanasema wimbo huo ni bahati kwao kwani umewafanya maarufu na kutambulika duniani lakini zaidi sana vipaji vyao kuwekwa bayana ni kama maajabu wao wanavyoona.

Saania na Muqqadas wanatokea katika familia masikini na walikuwa nje ya elimu mara baada tu ya masomo yao ya elimu ya awali .Hawaongei sana lugha ya kiingereza na ili kujifunza vyema wimbo huo, inawapasa huimba kwa sauti kubwa na kuyaweka maneno ya kiingereza katika lugha yao ya asili ya Urdu .

Televisheni nchini Parkistan waliwaalika kwenda kufanya nao mahojiano na hata kuimba wazi.

Bieber

Image caption Justin mwenyewe aliyeleta tofauti katika maisha ya mabinti hao

Justin Bieber alifanya tumbuizo la wimbo huo mnamo mwaka 2013 na mabinti hao wana tamani mno kukutana na Justin Bieber siku moja. Na kinachoendelea sasa katika maisha yao hawakukitarajia hata siku moja kuwa watakuwa maarufu duniani,kwasababu ya wimbo huo wamepanda ndege, wakahojiwa runingani kwa mara ya kwanz amaishani hayo yanawatokea ,na ilikuwa ni ndoto yao hatimaye.

Tulikuwa tukijionea maajabu, ati nywele zetu zinatengenezwa vizuri, tuna pakwa poda usoni ,nasi hatujawahi kwenda kwenye sehemu za urembo hata siku moja,kila kitu kwetu kilikuwa ni maajabu mno, hatujui nini kitatutokea hapo baadaye,anasema Saania huku akitabasamu.

Mama wa binti hao, Shahnaz Tabaydar anasema yeye pia ni shabiki mkubwa wa Justin Bieber.

Shahnaz anasema kwamba haamini kuwa yote hayo yanawatokea mabinti zake ,na anatoa shukrani zake kwa Justin Bieber. Anatamani siku moja binti zake wawe waimbaji wa kimataifa na watambe katika nchi za Pakistan and India. Na anaamini watapata msaada na uungwaji mkono wanaoutaka.

Mama huyu anaonesha masikitikiko yake dhahiri kuwa binti zake waliikosa elimu kutokana na umasikini mkubwa ulioko kwenye familia yake.ingawa hata leo mama Tabaydar anatamani binti zake warejee shuleni.

Baba wa mabinti hao hana kubwa la kusema zaidi ya kudai kuwa anaona fahari kwa hatua ambayo binti zake wameifikia maishani.

Nchi ya Pakistani imeshikilia msimamo mkali wa dini,na hata uwe na kipaji cha namna gani kuimba hadharani namna wafanyavyo binti zake si jambo la kawaida, ingawa mpaka sasa mabinti hao hawajakabiliana na upinzani wa namna yoyote.

Anasema mabinti zake wanafanya kitu ambacho mabinti wengine hawawezi kukifanya,lugha ya kiingereza ilikuwa ngumu kwa mabinti hao ,lakini hatimaye wameimudu lugha hiyo .

Na sasa Saania na Muqqadas wanataka kuizunguka dunia ,huku wakiwa na matumaini ya kuonana na Justin Bieber na kuimba pamoja naye.