Mtu anayelewa kwa kukula viazi karanga

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nick Hess kutoka ulaya anahitaji tu kiwango kidongo cha viazi kulewa chakari

Watu wengi wangependa kulewa bila kutumia hela zao kununua vileo.

Lakini Nick Hess kutoka ulaya anahitaji tu kiwango kidongo cha viazi kulewa chakari.

Nick anakabiliwa na hali nadra ya afya maarufu kama "Auto- Brewery Syndrome".

Hii inamaanisha kuwa yeye anaweza kulewa chopi kwa kula kifuko kizima cha viazi karanga.

Mkewe ameiambia BBC kuwa wakati mwengine huwa wanaweza kuwa chumbani wakila na kustarehe tu kwa kutizama Televisheni kisha mumewe anaanza kuwa mwenye matusi makali na kuropokwa maneno yenye aibu hata mbele ya wageni wao.

Awali walikuwa anamkaripia kwa utovu wa adabu lakini baada ya kipindi kirefu cha kuvumilia aligundua kuwa hakuwa ameondoka wala kunywa tembo kisri.

Alimpeleka hospitalini na ni huko alikoambiwa kuwa maskini mumewe alikuwa ''ni mgonjwa'' wala sio mlevi kama alivyodhaniwa.

Haki miliki ya picha
Image caption Chachu

"Auto- Brewery Syndrome"

Hii ni hali ambayo huwezesha tumbo la mgonjwa kugeuza chakula chenye wanga (Cabohydrate) tumboni kuwa na uwezo wa kulewesha kwani tumbo lake hutoa chachu (Yeast) kwa wingi ambayo hufanya chakula tumboni kugeuzwa tembo kwa haraka mno.

Katika hali yake Bwana Hess, tumbo lake linatoa Chachu maradufu mara 3 zaidi ya mwili wa kawaida.

Mkewe anaeleza jinsi alivyokuwa akisaka chupa za tembo zilizofichwa ndani ya nyumba bila mafanikio.

Kwa muda mrefu hakufahamu hasa kilichomkumba akisema kwamba anajipata mgonjwa bila sababu kwa kuumwa na tumbo na kichwa.

Marafiki na familia walianza kumtuhumu kwamba alikuwa mlevi kiasi .

Aliiambia BBC: "halikuwa jambo la kawaida, mara nyingi ningetamani kula viazi lakini punde tu nilipokula tu najiskia mlevi na kuamka asubuhi nakuwa na mchafuko wa roho.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nick Hess kutoka ulaya anahitaji tu kiwango kidongo cha viazi kulewa chakari

Watu walifikiria kwa ni mlevi licha ya kutotumia kileo chochote, ni wakati tu mkewe alipomnasa kwa kanda ya video na kudhibitisha kwamba hatumii vileo.

Mkewe, Daren Daw, anasema Hata baada ya kupimwa hospitalini kwa muda mrefu, shida hiyo iligunduliwa baada ya kumpa mmewe chakula kizito chenye wanga.

Mwaka wa 2010 alipewa glasi moja ya tembo lakini alipopimwa damu iligundulika kuwa tumbo la bwana huyo lilikuwa limechubua kileo sawana mtu aliyegonga glasi 7 za pombe kali ya Vodka.

Kwa sasa anapewa dawa ya kupambana na vimelea na kutumia vyakula kiasi venye wanga lakini bado anajipata melvi mara moja au mbili kwa mwezi