Polisi wavunja maandamano Mynmar

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Polisi watumia fujo kuvunja Maandamano Mynmar

Polisi wa kupambana na ghasia wametumia vitoa machozi kuutawanya umati wa wanafunzi uliokuwa ukiandamana kupinga sheria mpya wanayosema inakandamiza uhuru wa elimu.

Walioshuhudia wameiambia BBC kuwa wanafunzi kadhaa wamekamatwa baada ya muafaka wa makubaliano ulioapangwa

kati ya wanafunzi na wakuu wa elimu kuvunjika na waandamanaji wakijaribu kuvunja vizuizi vilivyowekwa na maofisa wa polisi.

Zaidi ya wanafunzi wapatao 150 walizuiwa katika mji wa Letpadan katika kati mwa Nchi hiyo tangu juma lililopita, baada ya maandamanao yao ya kuufikia mji wa Yangon.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi watumia fujo kupitia kiasi

Wanafunzi hao wamezuiwa na polisi wa kupambana na ghasia.

Maandamano hayo ya kupinga sheria hizo mpya ya Elimu yalianza mji wa Mandalay yapata mwezi mmoja uliopita.