Mke wa Gbagbo miaka 20 gerezani

Image caption Mke wa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Simone.

Mahakama nchini Ivory Coast imemhukumu aliyekuwa mke wa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, kifungo cha miaka 20 gerezani.

Simone Gbagbo amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 na 2011.

Simone Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake, aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu mjini The Hague Uholanzi.

Katika ghasia hizo watu takriban elfu tatu walifariki dunia.