Amnesty International yaikosoa Iran

Haki miliki ya picha
Image caption Watoto nchini Iran

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu, Amnesty International, limekosoa jaribio la Iran kuwahamasisha wanawake kuwa na watoto wengi.

Moja ya sheria inayopendekezwa itakuwa ni kinyume cha sheria kueneza habari juu ya uzazi wa mpango.

Suala jingine ni kwamba itakuwa ni vigumu kwa wanawake wasio na watoto kupata kazi na kufanya kuwa ngumu watu kuachana.

Shirika hilo la Amnesty International limesema sheria hizo zitakuwa ni kipingamizi kwa haki za wanawake. Hadi katika siku za karibuni Iran ilikuwa ikiunga mkono uzazi wa mpango, lakioni mamlaka nchini humo sasa zina wasiwasi kuhusiana na idadi ya watu wanaozeeka.