Internet yatumika kuuza watoto China

Haki miliki ya picha Xinhua
Image caption Mtoto wa kiume ambaye anadaiwa kuuzwa na daktari aliyemzalisha nchini China amerejeshwa kwa wazazi wake

Uchunguzi wa BBC umebaini kuwepo matangazo ya kuuzwa watoto nchini China kupitia mtandao wa interntet.

Baadhi ya matangazo hayo yanatolewa chini ya kisingizio cha kuasili licha ya jitihada za polisi kuzuia usafirishaji wa watoto.

Tangazo moja katika mtandao lilihusu mtoto wa kike mwenye umri wa miezi nane kwa mauzo ya dola elfu thelathini.

Ingawaje matangazo ya kuasili watoto yanaruhusiwa kisheria nchini China, matangazo kuhusu kuuza watoto ni makosa kisheria.

Inakadiriwa kuwa watoto elfu ishirini wanatekwa kila mwaka, wengi wanauzwa baadaye.(China haijapishi takwimu rasmi za matukio hayo).

Wnaopatikana na makosa ya kusafirisha watoto wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa lakini wanaharakati wanasema adhabu kali zaidi inahitajika kwa wale waliojitayarisha kununua watoto.

Mahitaji hayo yanapata msukumo wa wanandoa wasio na watoto.