Mbwa avalishwa na kutembea kama binadamu

Image caption Mbwa aliyevalishwa kama binadamu.

Mbwa aliyekuwa amevalia kama mwanadamu huku akitembea kwa miguu yake miwili amezua mjadala katika mitandao na watu kumgeukia kila kona anayokatiza hii imetukia huko Kusini Magharibi mwa China hasa jimbo Sichuan.

Mbwa huyo mwenye umri wa mwaka mmoja ambaye ni dume mwenye manyoya ya kutosha alionekana akiwa amevalia kofia,shati na sketi alikuwa akitembea huku mgongoni akiwa na begi la shule kwa hakika alikuwa na muonekano wa mwanafunzi mdogo wa jinsi ya kike.

Alikuwa na muonekano maridadi na mvuto hasa.Na huwezi kuamini kuwa anaweza kutembea kwa miguu miwili ya nyuma anasema mpita njia Luo.

Mmiliki wa mbwa huyo Zhu anasema ametumia muda wa muda wa mwezi mmoja kumfundisha mbwa huyo kutembea wima.Wakati akivalishwa nguo mbwa huyo alionekana kuwa mtulivu na kuruka ruka na ana uwezo wa kutembea kilomita mbili wima kama mwanadamu.

Zhu anasema alianza kumfundisha mbwa huyo kama kujifurahisha yapata miaka ishirini iliyopita na baada ya mafanikio hayo, anawafundisha mbwa wengine wengi na wa umri tofauti tofauti .