Manmohan atuhumiwa kwa ufisadi India

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mkuu wa zamani wa India Manmohan Singh akituhumiwa kwa ufisadi katika mauzo ya migodi ya makaa ya mawe akiwa madarakani

Waziri mkuu wa zamani wa India, Manmohan Singh ametakiwa kufika mbele ya mahakama mwezi uajo, kujibu tuhuma za kula njama na rushwa kuhusiana na kuzipa kampuni binafsi migodi ya makaa ya mawe.

Mahakama kuu ilitoa hukumu mwaka uliopita kuwa taratibu zilizotumiwa na serikali kuuza migodi ya makaa ya mawe zilikuwa na makosa.

Wizara ya makaa ya mawe imeshutumiwa kwa kuuza migodi kwa bei ya chini na kuisababishia hazina hasara ya mabilioni ya dola za Kimarekani.

Bwana Singh amekana kuhusika na tuhuma hizo.

Chama chake cha Congress kimeiongoza India kwa mwongo mmoja kutoka mwaka 2004 hadi mwaka uliopita.