Saa sawa na zile za Apple zauzwa China

Image caption Saa za Iwatch

Saa aina ya Smartwatches zinazofanana na zile za Apple zimeanza kuwekwa katika matangazo ya biashara katika mtandao nchini China.

Mtandao wa Alibaba Taobao umeziorodhesha bidhaa hizo zenye nembo ya AW08 na iWatch.

Zote zina taji la kidijitali lililo na vibonyezo kando ya uso wa saa hizo,pamoja na mikanda inayofanana sawa na saa za Apple zinazotarajiwa kuzinduliwa.

Hatahivyo orodha yake inaonyesha kwamba zinafanya kazi kupitia programmu ya Google Android badala ya programu ya Apple Watch OS.

Mbali na kwamba saa hizo sio za kampuni ya Apple, zinauzwa kwa Yuan 250 ambazo ni sawa na dola 40 ikiwa ni kiasi kidogo cha Yuan 2,588 ambazo saa za Apple zitauzwa nchini China punde tu zitakapozinduliwa..