Madona anasema vijana wanamfaa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mwanamuziki Maarufu wa nchini Marekani Madonna

Mwanamuziki maarufu wa kimarekani, Madonna ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mcheza dansi wake Brahim Zaibat aliyemzidi miaka 28 na Timor Steffens mwenye miaka 27 amesisitiza kuwa si kwamba anavutiwa na vijana wadogo isipokuwa ''hutokea tu'' kwa kuwa wanaume wengi wa umri wake hawapatikani.

Alipoulizwa kuhusu kuwa na mahusiano na vijana wadogo, aliliambia Gazeti la New York Daily kuwa ''hali hiyo hujitokeza tu wanaume wengi wa umri wangu wameoa na wana Watoto, mimi ni ni mtu mwenye kuthubutu''.alieleza

''Mimi ni Mama nisie na Mume.nina watoto wanne.ninamaanisha unatakiwa kuwa na uthubutu kuwa na maisha kama yangu.watu walio na umri mkubwa , huwa hawana uthubutu sawa na wadogo.''

Madonna mwenye umri wa miaka 56 ambaye awali aliolewa na Guy Ritchie ,46 ba Sean Pen,54 hivi karibuni amekiri atafunga ndoa ikiwa atampata mwanaume ''sahihi''.