Benki ya China yaitia wasiwasi Marekani

Image caption Fedha za China

Marekani imeelezea wasiwasi wake kufuatia uamuzi wa Uingereza kuwa nchi ya kwanza kuu ya magharibi kujiunga na benki ya uwekezaji ya China.

Marekani ina wasiwasi iwapo benki hiyo mpya itaweza kutimiza viwango vya kimataifa

Sasa Marekani imewataka washirika wengine wakiwemo Australia, Korea kusini na Japan kutofuata mkondo huo.

Waziri wa fedha nchini Uingereza George Osborne ameilezea benki hiyo kama fursa isiyo na upinzani kuwekeza katika soko linalobadilika.

Muhariri wa BBC nchini China amesema kuwa ni mpango wa China wa kutaka kupunguza ukiritimba wa Marekani katika mfumo wa fedha duniani.

China imefurahishwa na ombi hilo la Uingereza