Mume achomwa kwa kumkumbuka marehemu mkewe

Image caption Mume achomwa kwa kumkumbuka marehemu mkewe

Mwanaume aliyechomwa na maji moto kwa kumkumbuka marehemu mke wake wake amesema kuwa haoni haya kamwe kwa kitendo alichofanyiwa na mpenzi wake.

Ken Gregory, 65, anayetokea Peterborough, Uingereza amesema kuwa wanaume wanaopondwa kuteswa ama hata kupigwa na wake wao hawapaswi kuona haya.

Yamkini Gregory alikuwa amepanga kutembelea kaburi la mke wake kwa sababu ilikuwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake lakini hoja hiyo ikapingwa

na mke wake wakati huo Teresa Gilbertson, 60 .

Image caption Mume aliyechomkwa kwa kumkumbuka marehemu mke wake

Wawili hao waliteta na kupelekea Teresa kumwagia maji yaliyochemka.

Wawili hao Gregory na bi Gilbertson walikutana miaka 7 iliyopita baada ya kifo cha mpenzi mke wake wa mika 30, Maureen.

Lakini kilichozua ubishi na hatimaye janga ilikuwa ni wazo tu ambayo bi Teresia anasema aliona kama hapendwi tena na akaamua bora waachane iwapo

Bwana Gregory ataendelea kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya mpenziwake wa zamani japo ni Marehemu.

Image caption Wawili hao walipooana miaka7 iliyopita

Gilbertson aliondoka kwenda kupika chai lakini akarejea akiwa amefoka na buli la maji moto ambayo alimwagia mumewe kutoka nyuma.

went to make a cup of tea but returned with a jug of boiling water which she poured over his head from behind.

Bi Teresa sasa anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha maumivu na uchungu mwingi kwa mumewe ambaye amemtaliki.

Gilbertson atahukumiwa tarehe 24 Mach.