Majaji kadha wa Misri wastaafishwa

Majaji wa Misri Haki miliki ya picha BBC World Service

Duru za mahakama ya Misri zinasema kuwa mahakimu kama 40 wamelazimishwa kustaafu - inavoelekea kwa sababu wanaonekana kuwa wanaunga mkono Muslim Brotherhood.

Majaji kadha walitia saini taarifa kulaani hatua ya jeshi ya kumuondoa madarakani Rais Muislamu, Mohammed Morsi mwaka 2013.

Wengine walijiunga na kundi lilounga mkono Brotherhood kabla ya Rais Morsi kutolewa madarakani.

Sheria ya Misri inakataza majaji kujihusisha na siasa, lakini wanaharakati wanaotetea haki za kibinaadamu wanasema wakuu hawasemi kitu kuhusu wale mahakimu ambao wazi wanamuunga mkono rais wa sasa wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi.