Sanamu ya Gandhi yazinduliwa London

Sanamu ya shaba ya Mahatma Gandhi London Haki miliki ya picha bbc

Sanamu ya shaba ya mgombea uhuru wa India, Mahatma Gandhi, imefunuliwa rasmi mjini London katika medani ya bunge la Uingereza.

Mamia ya watu walihudhuria kutazama sherehe hiyo huku bendi ikipiga muziki wa Kihindi na bendera za India zikipepea.

Kwenye sherehe hiyo, Waziri Mkuu, David Cameron alimuelezea Gandhi kuwa kati ya watu mashuhuri kabisa katika historia ya siasa duniani; na alisema sanamu hiyo inampa makaazi ya daima nchini Uingereza.

Sanamu hiyo iko kando ya sanamu za viongozi wa zamani kama Winston Churchill, ambaye alipinga harakati za Gandhi kuania uhuru kutoka Uingereza.

Gandhi aliuliwa mwaka wa 1948 miezi michache baada ya India kupata uhuru.