Wapiganaji wa IS wazungukwa Iraq

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Iraq wamewazingira wapiganaji wa IS katika mji wa Tikrit

Wanajeshi wa Iraq pamoja na wanamgambo wa Ki-Shia wanaendelea kuwazingira wapiganaji wa Islamic State, ambao bado wanashikilia mitaa ya kati mwa mji wa Tikrit - mji wa kiongozi wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein.

Televisheni imeonyesha wanajeshi wa Iraq wakisaidiwa na wanagambo wa madhebu ya Shia wakishambulia maeneo ya IS mjini Tikrit kwa makombora

Kiongozi wa kundi moja la wanamgambo hao wa Ki-Shia alidai kuwa wapiganaji wa IS waliobaki mjini Tikrit hawazidi 70.

Lakini alisema inaweza kuchukua siku chache kuwashinda.

Tikrit iko ndani ya eneo linalodhibitiwa na IS, na waandishi wa habari wanasema ikiwa serikali itashinda huko, itakuwa pigo kubwa kwa wapiganaji hao.