Makamo rais S-Leone akimbilia ubalozini

Makamo wa rais wa Sierra Leone Sam-Sumana Haki miliki ya picha AFP

Makamo wa rais wa Sierra Leone, Samuel Sam-Sumana, anasema kuwa anaomba hifadhi katika ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown.

Hayo yanafuatia ripoti kuwa wanajeshi wameizingira nyumba yake na kuwanyang'anya silaha walinzi wake.

Juma lilopita, Bwana Sam-Sumana alitolewa katika chama tawala cha APC akishutumiwa kuwa alichochea fujo, alikuwa na shahada za masomo za uongo, na kusema uongo kuhusu dini yake.

Mwisho wa mwezi wa Februari alijiweka karantini baada ya mlinzi wake mmoja kufariki kwa sababu ya Ebola.

Alisema kuwa atajitenga na watu wengine kwa siku 21.