Mke wa Agathon Rwasa ashambuliwa Burundi

Image caption kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa

Watu waliokua na Silaha wamemjeruhi mke wa kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa.

Mama huyo alikua kwenye Saloon wakati watu hao walipoivamia na kuanza kufyatua risasi.

Mwandishi wa BBC Mjini Bujumbura anasema visa vya uhalifu vimeongezeka nchini humo.

Ameongeza kwamba mashambulio mengi hasa yameonekana kuwalenga viongozi wa upinzani.

Haijabainika waliotekeleza shambulio hilo ni akina nani.