Mancity yalazwa na Burnley

Image caption Mchezaji Goerge akiifungia Burnley bao la pekee dhidi ya Mancity

Bao la George Boyd liliipatia kilabu ya Burnley ushindi dhidi ya Mancity na hivyobasi kutia doa harakati za klabu hiyo kuhifadhi taji lake la ligi ya Uingereza.

Boyd alifunga baada ya beki wa kilabu ya Mancity Vincent Kompany kushindwa kuokoa hatari katika lango la City.

Mancity ilipoteza fursa nyingi za kujiweka kifua mbele huku mkwaju uliopigwa na Edin Dzeko ukiokolewa na Tom Heaton naye Sergio Aguerro akikosa kichwa kizuri cha wazi.

Pablo Zabaleta aliangushwa kunako dakika za mwisho za mechi hiyo kukamilika lakini refa akakataa kutoa penalti licha ya wachezaji wa City kulalamika.