Vatican:Nguvu zitumiwe dhidi ya IS

Image caption Askofu mkuu wa Vatican Silvano Tomasi

Makao makuu ya kanisa katoliki duniani Vatican yanasema kuwa nguvu inaweza kutumiwa kusitisha mashambulizi yanayoendeshwa na wanamgambo wa Islamic State dhidi ya wakristo na makundi mengine madogo .

Askofu mkuu Silvano Tomasi ambaye ni mwakilishi mkuu wa Vatican kwenye umoja wa mataifa mjini Geneva ameyashutumu makundi ya jihad kwa kuendesha mauaji ya halaiki.

Akizungumza kupitia mtandao wa Vatican amesema kuwa hatua za kijeshi zitaanzishwa ikiwa suluhu ya kisiasa haitapatikana.

Lakini amesema kuwa muungano wowote dhidi ya Islamic State ni lazima ujumuishe nchi za kiislamu kutoka mashariki ya kati.