Israeli:Chama cha Netanyahu taabani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amewaomba wafuasi wake kuzuia serikali ya mrengo wa kushoto kuingia madarakani katika uchaguzi wa hapo kesho Jumanne.

Alikuwa akihutubia mkutano wa kisiasa wa wafuasi wa vyama vya mrengo wa kulia mjini Tel Aviv.

Netanyahu amesema kuna hatari kubwa kwamba serikali ijayo itaundwa na muungano wa kizayonisti ya mrengo wa kushoto.

Kura ya kutafuta maoni inaashiria kwamba muungano huo unaoongozwa na Isaac Herzog na Tzipi Livni.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Muungano unaongozwa na Tzipi Livni unatarajiwa kuushinda ule unaoongozwa na waziri mkuu wa sasa Benjamin Netanyahu

Muungano huo huenda ukashinda viti vinne zaidi bungeni kukishinda chama cha Netanyahu cha Likud.

Mwandishi wa BBC anasema Netanyahu ametumia mkutano wa jana wa kisiasa kuwakumbusha wapiga kura

kile anachokiona kuwa ndio kitetezi chake kikuu cha uchaguzi - kutoteteleka kwake kwa masuala yanayohusu usalama wa kitaifa.