Uchaguzi: Israeli yaamua

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mamilioni ya wapiga kura wakipiga foleni katika kituo cha kupigia kura

Mamilioni ya wapiga kura wamejitokeza leo kuchagua wabunge wapya nchini Israeli.

Uchaguzi huo unaushindani mkali ukilinganishwa na chaguzi za awali nchini Israeli.

Waziri mkuu wa sasa Benjamin Netanyahu, anatafuta muhula wa nne na kufanya kuwa mmojawepo wa viongozi wachache kuwahi kushikilia cheo hicho kwa muda mrefu zaidi.

Kwa mjibu wa kura ya maoni ya uchaguzi mkuu, yaliyotolewa majuzi, Chama cha Likud cha Waziri mkuu Netanyahu kinafuatia kile cha muungamo wa chama cha mrengo wa kati na kushoto.

Image caption Netanyahu akitumbukiza kura yake

Kampeini imekuwa ikilenga usalama wa kitaifa, hasa kuhusiana na hatari ya mpango wa kinuklia wa Iran na kuongezeka kwa makundi ya wanamgambo wa kiislamu.

Wakati huo huo, muungano wa chama cha Zionist, wakiongozwa na Yitzhak Herzog na Tzipi Livni, wameamua kushughulikia maswala ya kijamii na uchumi wa taifa,

maswala yanayowakumba moja kwa moja raia wengi wa Israeli.

Akipiga kura yake katika kituo kimoja mjini Jerusalem, Rais wa Israel, Reuven Rivlin, aliwaomba waisraeli wote kujitokeza kwa wingi kupiga kura

Image caption Viongozi wa muungano wa chama cha Zionist, wakiongozwa na Yitzhak Herzog na Tzipi Livni

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hakuna chama kilichowahi kushinda zaidi ya asilimia 50 ya kura kutokana na mfumo wa kura za uwakilishi zinazotumika nchini humo.

Kutokana na sera hiyo wadadisi hawatarajii kuwa chama chochote kitaibuka na zaidi ya robo ya kura zote katika uchaguzi huu.

Waziri mkuu bwana Netanyahu aliitisha kura za mapema kwa nia ya kushinda asilimia kubwa ya viti na hivyo kuwa na muungano dhabiti kuliko ule aliokuwa nao.