Pigo kwa Muslim Brotherhood Misri

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi mwandamizi wa kundi la Muslim Brotherhood lililopigwa marufuku nchini Misri, Mohammed Badie amehukumiwa adhabu ya kifo

Mahakama nchini Misri imemhukumu adhabu ya kifo kiongozi mwandamizi wa kundi la Muslim Brotherhood, Mohamed Badie na wanachama wengine muhimu kumi na watatu wa kundi hilo lililopigwa marufuku nchini humo.

Wote kumi na wanne wamepatikana na hatia ya kupanga mashambulio dhidi ya serikali. Bwana Badie amekuwa akikabiliwa na mashitaka kadha. Alihukumiwa adhabu ya kifo katika kesi nyingine zilizopita kabla lakini adhabu zilipunguzwa kuwa kifungo cha maisha jela.

Mahakama za Misri zimewahukumu mamia ya watu wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood adhabu ya kifo baada ya kesi zilizoendeshwa haraka haraka nakukosolewa na vikundi vya kutetea haki za binadamu na serikali za nje.

Muslim Brotherhood ilitangazwa kuwa kundi la kigaidi mwaka 2013.