Ni misikiti 19 pekee iliosalia CAR

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Msikiti wa jamhuri ya afrika ya kati

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa anasema kuwa karibia misikiti yote katika jamhuri ya Afrika ya kati imeharibiwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe viliovyoanza miaka miwili iliopita.

Samantha Power ambaye alilitembelea taifa hilo wiki iliopita amesema kuwa ni misikiti 19 pekee kati ya 436 iliosalia.

Vita vingi vimekuwa kati ya waislamu na wakristo.

Bi Power ameonyesha wasiwasi kuhusu ukosefu wa usalama huku vikosi vya Ufaransa na vile vya muungano wa Ulaya vikiondoka nchini humo kabla ya kikosi kamili cha Umoja wa mataifa kupelekwa.