Upinzani wampongeza Netanyahu Israel

Image caption Kingozi wa Upinzani nchini Israel Yitzhak Hertzog amempongeza waziri mkuu Netanyahu kwa ushindi wa chama cha Likud

Kiongozi wa upinznai nchini Israeli Yitzhak Hertzog amempongeza Benjamin Netanyahu kwa ushindi wake katika uchaguzi wa ubunge nchini humo na kumtakia kila la kheri.

Netanyahu anelekekea kushinda nafasi ya kuhudumu kwa mara ya tatu kama waziri mkuu wa Israeli na hatamu yake ya nne kwa jumla.

Chama chake cha Likud kimepata ushindi wa asilimia 24 ya kura zilizopigwa dhidi ya asilimia 19 ya chama cha mrengo wa kushoto - Zionist Union.

Sasa Netanyahu analenga kuunda serikali thabiti na imara ya mseto na vyama vidogo vya mrengo wa kulia.

Katika kampeni yake ya kuwania kuchaguliwa kwa awamu ya tatu alisisitiza kuhusu usalama wa kiatifa wa Israel.

Akizungumza na wafuasi wake, bwana Netanyahu amewashukuru kwa jitihada zao za kumuunga mkono.