Kanye West amuanika mkewe mtandaoni

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mkewe Kanye West Kim Kardashian ambaye picha zake za utupu ziliwekwa katika mtandao wa Twitter

Msanii wa muziki Kanye West ameweka msururu wa picha za utupu wa mkewe Kim Kardashian West katika mtandao wake wa Twitter.

Nyota huyo wa muziki wa rap aliwagawia picha hizo takriban watu millioni 11.7,wanaomfuata katika mtandao wa twitter pamoja na ulimwengu mzima.

Picha hizo zinamuonyesha mkewe Kim kardhashian akijiziba uchi wake na mikono.

Katika ujumbe wake msanii huyo aliyeimbia wimbo kwa jina ''Yeezus'' alijigamba kuhusu hatua zilizopigwa na mkewe katika Runinga ya Reality TV na kusema ana bahati kuwa naye.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kim Kardashian

Katika ujumbe mmoja ambao uliwekwa na picha ya uchi ya Kardashian akijiziba kifua chake na mikono,Kanye West aliandika ''NINA BAHATI''.

Ujumbe huo ulifuatiwa na mwengine pamoja na picha ya Kim ukimpongeza Kardashian kwa kupata watu millioni 30 katika mtandao wake wa kijamii.