Upendeleo maalum,usawa kwa wote

Image caption Waziri Waiguru

Kenya iko katika njia sahihi kisheria na inatambua umuhimu wa usawa kati ya wanaume na wanawake na inahimiza taifa lizingatie hatua za upendeleo maalum ili kuhakikisha kwamba usawa wa kijinsia unaafikiwa. Hiyo ni kauli ya waziri wa Ugatuzi na mipango nchini Kenya Anne Waiguru katika mahojiano maalum na Idhaa hii.

Bi. Waiguru ambaye anahudhuria mkutano wa 59 wa Kamisheni ya hali ya wanawake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York amesema..“Tuko katika njia sahihi lakini hatupaswi kubweteka kwani juhudi zetu za kuimarisha wanawake kiuchumi zinaibua uongozi kimataifa na kwa hiyo tunahitaji kuhakikisha kwamba ustawi wa wanawake unaendelezwa sawia na maswala mengine ya kijamii na kisiasa.”

Ameongeza kwamba ni kwa mantiki hiyo ambapo serikali imetenga mfuko maalum kwa ajili ya kuyawezesha makundi maalum katika jamii wakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Kufuatia uamuzi huo serikali imetenga asilimia 30 ya zabuni zote za umma nchini Kenya ambayo ina thamani ya takriban dola bilioni 2.4 kwa mwaka kwa ajili ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.