Usalama:Japan na China kukutana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa China Xi Jinping akimsalimia waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.Jap[an na China zinatarajiwa kukutana hivi karibu kwa mkutano wa usalama

China na Japan wanafanya mkutano wa kwanza wa kiwango cha juu wa usalama katika muda wa miaka minne.

Mkutano huo unaofanyika Tokyo unajumuisha maafisa kutoka wizara za mambo ya nje na ulinzi.

Mazungumzo hayo yalisitishwa mnamo mwaka 2011 kutokana na hofu kuhusu visiwa vinavyozozaniwa mashariki mwa bahari ya China.

China inasema Japan imeshindwa kuomba msamaha kwa uchokozi wake wakati wa vita vya dunia vya pili.

Pande zote zimesisistiza umuhimu wa mazungumzo ya kweli kudumisha amani.