Raia wa S Leone kutotoka nje kwa siku 3

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ebola nchini Sierra Leone

Katika harakati za kuangamiza kabisa janga la ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, taifa hilo linasema kuwa juma lijalo litawazuilia karibu watu milioni mbili unusu majumbani mwao kwa siku tatu.

Msemaji wa serikali ameiambia BBC kuwa shughuli hizo zitaanzia mji mkuu Freetown na kazkazini mwa nchi hiyo, kati ya Machi 27 na 29.

Wafanyikazi wa kimatibabu watazuru kila nyumba ili kubaini dalili za ugonjwa huo, huku wakiwakumbusha wananchi hatari ya kushika maiti na kuwapeleka wagonjwa wa ebola kwa madktari wa tiba ya kiasili.

Visa vya Ebola vinaripotiwa kila juma nchini Sierra Leone na Guinea.

Kufikia sasa hakuna kisa chochote cha ugonjwa huo ambacho kimeripotiwa nchini Liberia, katika kipindi cha majuma matatu yaliyopita.