Makao ya rais yashambuliwa Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Abd Rabbuh Mansour Hadi

Rais wa Yemeni Abd Rabbuh Mansour Hadi amehamishwa hadi mahala salama baada ya mashambulio ya angani katika maskani yake katika mji wa Aden, Kusini mwa taifa hilo.

Bwana hadi alitoroka kutoka mji wa Sanaa ambao umetekwa na Waasi wa Houthi na anajaribu kujenga kambi mpya ya utawala katika eneo hilo.

Ndege mbili za kivita zinaaminika kutumika katika mashambulio hayo, lakini maskani yake hayakushambuliwa moja kwa moja.

Ndege hizo zinadaiwa kutumwa kutoka mji wa Sanaa.

Uvamizi huo ulitokea saa chache baada ya jeshi la Hadi kutibua shambulizi katika uwanja wa ndege wa kimataifa lililotekelezwa na vikosi vitiifu vya Houthi.