YAHOO kufunga afisi zake China

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yahoo kufunga afisi zake nchini China

Kampuni ya mtandao YAHOO inatarajiwa kufunga afisi yake ya mwisho katika eneo la China bara.

Kampuni hiyo kama kampuni nyengine za kiteknologia imekuwa ikikabiliwa na ushindani mkubwa nchini Uchina kutoka kampuni nyengine za mtandao.

Takriban ajira 300 zitapotea.

Yahoo ilisitisha utoaji wa huduma za kutuma ujumbe kwa kutumia njia ya Email kwa wateja wake nchini Uchina mnamo mwaka 2013.

Katika taarifa yake,kampuni hiyo imesema kuwa inaunganisha baadhi ya huduma zake ili kuimarisha ushirikiano.