Mtoto wa miaka 12 ataka kumuua mamake kisa ?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mtoto wa miaka 12 ameshtakiwa kwa jaribio la kumuua mamake kwa kumpokonya iphone

Mtoto wa miaka 12 amewashtua wengi baada ya kujaribu kumuua mamake mara mbili kwa sababu alimpokonya simu yake ya Iphone.

Kulingana na afisa anayesimamia usalama katika jimbo la Colorado Marekani mtoto huyo alimtilia sumu mamake kwa nia ya kulipiza kisasi.

Mamake aliripotiwa kuzidiwa hali Machi tarehe mbili baada ya kubugia mchanganyiko wa maziwa na barafu''smoothie'' lakini ikabainika kuwa mchanganyiko huo ulikuwa umetayarishwa kwa aina ya sabuni majimaji.

Mamake aliwaambia maafisa wa polisi kuwa alipigwa na bubumbuazi aliponusia harufu ya sabuni baada ya kunywa mchanganyiko huo uliotayarishwa na mwanawe.

''mara ya kwanza nilidhania kuwa hakusuza vizuri glasi aliyoniandalia nayo lakini baada ya hapo akapata sabuni hiyohiyo katika buli lake la maji ndipo akagutuka''alisema mama huyo

Mwanawe alimwambia kuwa alikuwa ameudhika sana na haua yake ya kumpokonya Iphone na kuwa alikuwa amefanya jaribio mbili ya kumtoa uhai.

Mamake alikimbizwa hospitali iliyokaribu ya mji wa Boulder kabla ya kuwaita maafisa wa polisi na kutoa ripoti hiyo.

Uchunguzi uliofwatia ukiongozwa na na sajini Bill Crist ulibaini nia ya mtuhumiwa kwa mjibu wa jarida la BuzzFeed .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtoto huyo ameshtakiwa kwa jaribio la kumua mamake

Mtoto huyo alikamatwa tarehe 20 Machi na kufikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya watoto alikoshtakiwa kwa jaribio la kumtoa uhai mamake .

ÔÇťamejaribu mara kadha kumtoa uhai mamake '' alisema sajini Crist.

Mamake kwa sasa ameruhusiwa kurejea nyumbani lakini bila shaka akiwa mwangalifu zaidi.

Idara ya haki katika jimbo hilo inaendelea na uchunguzi.