USA:Netanyahu amekiuka mpango wa amani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Marekani yasema israel imekuka dhamira ya mpango wa amani

Msemaji wa serikali ya Marekani, Josh Earnest, amesema waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekiuka dhamira yake ya awali ya kuundwa kwa mataifa mawili kama suluhu ya mgogoro wa Israel na Palestina mwanzoni mwa wiki hii, na kwamba Marekani inautathmini msimamo wake upya.

Matamshi ya waziri mkuu huyo wa Israel ya kutotaka kuwepo kwa taifa la Palestina yanaonekana na wengi kama ndio yaliyomsaidia kushinda katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne.

Netanyahu amekiambia kituo cha televisheni cha Marekani, MSNBC, kwamba bado anabaki na dhamira ya kuundwa kwa taifa la Wapalestina, huku akikana taarifa za kubadili msimamo katika sera yake.

Bwana Netanyahu ameiambia MSNBC kwamba anataka Marekani na Israel kuendelea kuwa washirika wakubwa: