Kenya Airways yapunguza safari zake TZ

Image caption Kenya Airways

AirwaysShirika la ndege la Kenya, Kenya Airways leo limeanza rasmi kupunguza safiri zake katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo la mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika hilo kupunguza safari zake kutoka 42 kwa wiki hadi 14.

Image caption Kenya Airways

Serikali ya Tanzania inasema huo ndio mkataba wa tangu awali na kulaumu mamlaka ya anga nchini Kenya kwa kushindwa kuafikia maelewano na mamlaka ya Tanzania kuhusu jambo hilo.

Tayari baadhi ya wasafiri wanaotumia ndege za shirika hilo wameanza kuathirika kufuatia shirika hilo kufuta baadhi ya safari kutoka Dar es Salaam