China, Japan na Korea kusini kukutana

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mawaziri wa kigeni kutoka Japa,China na korea kusini

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa China, Japan na Korea kusini wanakutana mjini Seoul leo jumamosi katika mkutano wao wa kwanza tangu miaka mitatu iliyopita.

Mazungumzo yao yanaratarajiwa kuangazia jinsi ya kuzuia misukosuko eneo hilo inayotokana na tofauti za kidiplomasia na mipaka.

Nchi hizo tatu zina uhusiano mkubwa wa kiuchumi lakini China na Korea Kusini zinaonekana kujitenga na Japan miaka ya hivi karibuni.

Kabla ya mkutano huo msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni nchini China alielezea matumaini yake kuwa mawaziri hao wataichukulia historia kama kioo na kuangazia mbele.