Kisa kipya cha Ebola chapatikana Liberia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mgonjwa wa Ebola Yardolo akituhusiwa kwenda nyumbani

Kisa kipya cha ugonjwa wa ebola kimegunduliwa nchini Liberia wiki chache kabla ya nchi hiyo kutangazwa kuwa isiyokuwa na ugonjwa huo.

Mkuu wa kundi linalohusika na kudhibiti ugonjwa wa ebola nchini humo ameiambia BBC kuwa mwanamume mmoja ambaye alipelekwa kwenye kituo cha matibau siku ya alhamisi alipatikana akiwa na ugonjwa wa ebola.

Wiki mbili zilizopita mgonjwa wa mwisho wa ugojwa wa ebola (Beatrice Yardolo) aliruhusiwa kuondoka hospitalini kwenye mji mkuu wa nchini hiyo Monrovia.

Liberia ilikuwa imesalia na siku 40 kabla ya kutangazwa kuwa isiyo na ugonjwa wa ebola kulingana na taratibu za shirika la afya duniani WHO.

Zaidi ya watu 4000 wameaga dunia nchini Liberia kutokana na ugonjwa wa ebola.