Mancity yaicharaza West Brom 3-0

Haki miliki ya picha EPA
Image caption mancity

Mshambuliaji wa Mancity Wilfried Bonny alifunga bao lake la kwanza na kuiweka kifua mbele Mancity baada Gareth McAuley kupewa kadi nyekundu.

Fernandinho na David Silva waliongeza mabao mengine mawili na kuisaidia City kupunguza idadi ya pointi kati yake na viongozi wa ligi Chelsea kuwa tatu hadi pale kikosi hicho cha Jose Mourinho kitakapocheza mechi zake mbili.

Hatahivyo mechi hiyo iliangazia sana kutolewa kwa mchezaji McAuley baada ya sekunde 89 pekee,ikiwa ni uamuzi wa mapema sana kufanywa katika ligi ya Uingereza msimu huu,ilipobainika kwamba refa Neil Swarbrick alitoa kadi

nyekundi kwa mtu ambaye hakustahili.