Arsenal yailaza Newcastle

Image caption Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud akisherehekea na wenzake baada ya kufunga mabao mawili

Arsenal ilihimili kishindo cha Newcastle katika kipindi cha pili huku ikiendelea na harakati zake za kuchukua nafasi ya pili katika jedwali la ligi ya Uingereza baada ya kupata ushindi wa sita mfululizo.

Baada ya Mancity kuicharaza West Brom ,Olivier Giroud alifunga mabao mawili katika dakika nne na kuiweka Arsenal kifua mbele huku timu hiyo ikitawala kila safu ya mchezo.

Giroud alifunga bao la kwanza baada ya krosi nzuri kutoka kwa Carzola kabla ya kufunga kupitia kichwa baada ya kona iliopigwa na hivyobasi kupata bao lake la 17 msimu huu.

Bao la Moussa Sissoko hatahivyo liliimarisha matumaini ya Newcastle lakini kipa David Ospina wa Arsenal alilazimika kufanya kazi ya ziada huku akimyima bao la wazi Remy Cabella.