Ennadha:Vita vya Libya ni tishio Tunisia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa Chama cha Ennadha nchini Tunsia Rache Ghannouchi kulia

Kiongozi wa chama cha kiislamu chenye msimamo wa wastani nchini Tunisia Ennadha anasema kuwa nchi hiyo itaendela kukabiliwa na vitisho ikiwa taifa jirani la libya litaendelea kukumbwa na mzozo.

Rached Ghannouchi alikuwa akizungumza na BBC baada ya watu waliokuwa wamejihami kuwaua watu 23 wengi watalii wa kigeni kwenye makavazi ya Bardo mjini Tunis.

Kundi la Islamic State lilisema kuwa wapiganaji wake waliendesha mashambulizi hayo.

Wapiganaji hao wanaripotiwa kupata mafunzo nchini Libya.