Mto Nile:Mazungumzo yatatupa suluhu

Image caption Al-Sisi alikuwa akizungumza jijini Addis Ababa, Ethiopia katika siku yake ya kwanza ya ziara rasmi nchini humo.

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi anasema mashauriano ndio suluhu ya pekee ya kutatua mzozo wa muda mrefu na Ethiopia kuhusu utumizi wa maji ya mto to Nile.

Al-Sisi alikuwa akizungumza jijini Addis Ababa, Ethiopia katika siku yake ya kwanza ya ziara rasmi nchini humo.

Hii ni mara ya kwanza katiuka muda wa miongo mitatu kwa rais yeyote wa Misri kutembelea Ethiopia na inajiri kufuatia mzozo wa kidiplomasia uliosababishwa na ujenzi wa bwawa kubwa katika mto Nile.

Mwandishi wetu wa Ethiopia Emmanuel Igunza na mengi zaidi.

Ziara ya Al Sisi inajiri siku moja tuu baada ya Misri, Ethiopia na Sudan kutia siani mkabata wa awali wa jinsi ya kugawanya maji yam to huo unaopitia mataifa yote matatu.

Kwa muda mrefu sasa Misri imepinga ujenzi wa bwawa kubwa la umeme katika mto Niule ikisema itatishi chanzo chake cha maji.

Akizungumza katika mkutrano wa pamoja jijini Addis Ababa, Rais Al-Sisi amesema mkataba ho uliotiwa saini jijini Khartoum Sudan ni hatua ya kwanza katika kutuliza hofu ya raia wa Misri kuhusu maji ya Nile.

“kwa kuchukua hatua tuliyoichukua tunanuia kuimarisha ushirikiano na kuaminiana baina ya mataifa yetu na Misri na Ethiopia Hivyo ndivyo tutakavyoimarisha maisha ya watu wetu''.

Image caption Ethiopia inasema bwawa hilo litaisaidia kuzalisha kawi

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn kwa upande wake amekariri kuwa bwawa hilo haliathiri kwa vyovyote viwango vya maji katika mataifa mengine yanayotegemea mto huo.

“Ufanisi muhimu zaidi tukiyopata ni nia ya kisiasa ya pande zote mbili na kujitolea kuendeleza uhusiano huu kwa manufaa ya watu wetu na kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Ni mahusiano ya kihistoria. Na nadhani tumefikia awamu ambapo tunaaminiana na kuelewana vyema.”

Wakati huohuo, mataifa kumi yanayonufaiki na mto Nile yamepongeza makataba huo uliotiwa saini na Misri, Ethiopia na Sudan.

Chini ya shirika la Nile basin Inititive, mataifa hayo yanayojumuisha Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

yanasema maelewano kama hayo ni muhimu katika kuhakikisha maendeleo katia kanda hii.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Viongozi hao wakionyesha umoja baada ya kutia sahihi mkataba

Bwawa hilo litakapokamilika mwaka wa 2017, litazalisha takriban megawati 6000 za umeme.

Itagharimu zaidi ya dola bilioni nne.

Chini ya mkataba wa enzi za kikoloni, Misri ilikabidhiwa uwezo wa kupinga miradi yoyote ya ujezni katika Mto huo.

Lakini Ethiopia ilikuwa miongoni mwa mataifa mengine kumi yaliyopinga mkataba ho na kutia saini makubaliano mengine mwaka wa 2013.