Ugiriki na Ujerumani wajadili madeni yao

Haki miliki ya picha z
Image caption Waziri mkuu mteule wa Ugiriki Alexis Tsipras

Viongozi wa Ujerumani na Ugiriki wakutana ujerumani kuinusuru ugiriki dhidi ya mzigo wa madeni.,huku waziri mkuu mteule wa Ugiriki akitoa onyo juu ya mahitaji muhimu ya msaada wa haraka wa kifedha.

Taarifa zinaeleza kuwa waziri Alexis Tsipras wa Ugiriki amemweleza kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwamba bila msaada mpya wa kifedha kutoka umoja wa ulaya, serikali yake haitaweza kuwa na uwezo wa kulipa madeni yake.

Waziri Tsipras ambaye anafanya ziara yake ya kwanza mjini Berlin alipokelewa na mwenyeji wake kansela Angela Merkel kwa gwaride la kijeshi la katika himaye ya chansela huyo.

Viongozi hao Waziri Mkuu wa Ugiriki na chansela wa Ujerumani wameelezea uhumimu wa nchi zote mbili kufanya kazi pamoja kufuatia mazungumzo ya Berlin kuhusu namna ya kukabiliana na madeni ya Ugiriki.

Chansela Angela Merkel amesema nchi zote mbili zinapaswa kuishi na kufanya kazi pamoja.

Pamoja na yote hayo jambo kubwa ni ushirikiano tulionao baina yetu na msingi mkubwa ni uaminifu.Kwa pamoja tumeweza kuainisha mambo yanayotatiza nchi hizi mbili,mambo ambayo tuna mtazamo nayo tofauti.

Lakini moyo wa ushirikiano wetu unatiwa msukumo na jambo hili,sote tunataka kufanya kazi pamoja,na nchi zote mbili ni mwanachama wa umoja wa ulaya na pia mwanachama wa NATO.

Naye waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras , amesema nim muhimu zaidi kwa Athens na Berlin kufanya mazungumzo ya pamoja kuliko kila mmoja kumzungumzia mwenzake.

Mkutano huu ni wa muhimu kwa kila mmoja kumfahamu mwenziwe kwa ufasaha.na hakukuwa na njia zaidi ya hii ya mazungumzo kwa njia ya mjadala.