Nyota wa 'Empire' wadaiwa kuwa wapenzi

Image caption Nyota wa filamu ya Empire Andre Lyon na Anaika Calhoun kama wanavyojiita katika filamu hiyo sasa wamdaiwa kuwa wapenzi katika maisha yao ya kawaida

Nyota wawili wa filamu ya 'Empire' Adre Lyon na Anika Calhoun ni watu wa familia moja katika filamu hiyo lakini katika maisha ya kawaida wawili hao wamedaiwa kuwa wapenzi.

Kulingana na mtandao wa TMZ nchini Marekani wawili hao walionekana katika harusi moja wakiwa pamoja na wengi waliohudhuria sherehe hiyo ya kukata na shoka wanasema nyota hao walionekana kupendana.

Katika filamu hiyo ya Empire ambayo ni filamu ya msururu iliyowavutia wengi mwaka huu wawili hao wanaigiza kama mtoto na mama yake wa kambo.