Ebola:Raia wa S Leone kusalia majumbani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia wa Sierra Leone waanza kusalia majumbani kwa siku tatu kwa lengo la kukabiliana na ebola

Mamlaka nchini Sierra Leone imeanza kutekeleza hatua ya kutotoka kwa siku tatu miongoni mwa raia wake itakayosaidia kukabiliana na kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa wa ebola.

Takriban watu millioni sita wametakiwa kusalia majumbani mwao kwa kipindi cha siku tatu huku watu wa kujitolea wakitembelea nyumba hadi nyumba kuwasaka watu walio na ishara za ugonjwa huo huku wakiwashauri wengine jinsi ya kuepuka maambukizi.

Visa kadhaa bado vinaendelea kuripotiwa kazkazini na Magharibi mwa Sierra Leone kila wiki.

Mataifa matatu ya Afrika Magharibi yalioathiriwa vibaya na Ebola Sierra Leone,Liberia,Guinea-yameweka lengo la kutokuwa na hata kisa kimoja cha ebola ifikiapo katikati ya mwezi ujao.