Nigeria:Jeshi laichukua ngome ya B Haram

Haki miliki ya picha
Image caption Jeshi la Nigeria lauteka mji wa Gwoza

Jeshi la Nigeria linasema kuwa limeuchukua mji wa kazkazini mashariki wa Gwoza unaoaminika kuwa ngome kuu ya Boko Haram.

Ni katika eneo hilo ambapo wapiganaji wa Boko Haram walitangaza uongozi wa kiislamu na ni miongoni mwa miji mikuu iliotekwa na kundi hilo katika kipindi cha hivi karibuni.

Tangazo hilo linajri siku moja tu kabla ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Uchaguzi huo uliahirishwa kwa mda wa wiki sita ili kutoa fursa kwa jeshi la muungano wa mataifa kupata mda zaidi wa kukabiliana na Boko Haram.

Rais wa Chad,taifa ambalo ni miongoni mwa yale yaliyo na vikosi vyake amesema kuwa vikosi vya Nigeria havijajizatiti.